Ajali iliyohusisha gari la kanisa yaua nane, yajeruhi 19

NA DIRAMAKINI

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 8 na majeruhi 19 katika ajali ya gari aina ya Coaster T 287 CCY mali ya Kanisa Katholiki Njombe iliyogongana na lori la makaa ya mawe.
Watu hao ni miongoni mwa vijana wa Umoja wa Vijana wa Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe (UVIKANJO) ambao walikwenda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila wilayani Njombe.
Ajali ilitokea jana majira ya jioni katika eneo la Igima wilayani Wanging'ombe Barabara Kuu kuelekea mkoa wa Ruvuma.
Aidha, amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mji wa Njombe Kibena pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa huo.

Post a Comment

0 Comments