Diamond Platnumz atoa milioni 10/- kuendeleza vituo vya Madrasa Dodoma

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI ya Wasafi Media imetoa shilingi milioni 10 kwa ofisi Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Dodoma ili kuendeleza vituo vya mafunzo ya Kiislam (Madrasa).

Akizungumza leo Aprili 27,2022 jijini Dodoma kwenye tukio la la fadhila za Ramadhani Iftar lililofanyika katika viwanja vya Bunge jijini humo, Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media, Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) amesema fedha hizo zitakwenda kusaidia kununua vitabu vya kusomea,busati na mikeka kwa ajili ya kuswalia.
Bw.Nasibu amekabidhi fedha hizo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Tulia Ackson ambapo Spika amemkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu.

Post a Comment

0 Comments