Mwanadaispora Chris Lukosi awapa Watanzania mbinu za kupiga fedha kipindi hiki cha uhaba wa mafuta duniani kupitia kilimo cha Canola (rapeseed)

NA DIRAMAKINI

Anaandika, Mwanadaispora Chris Lukosi ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Uingereza na muuzaji maarufu wa zana mbalimbali za kilimo, magari na nyinginezo kutoka nchini humo.

....KAMWENE NDUGU ZANGUNI, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana mjadala wa mafuta unaoendelea nchini na nimegundua tunapokosea mpaka kupelekea uhaba wa mafuta ya kula.
Ndugu zangu, kama mjuavyo mafuta yanayotumiwa sana nyumbani ni mafuta ya vegetable oil, na kwa nyumbani tumekariri sana kuwa vegetable oil ni mafuta ya alizeti tu au mabangayeye.

Kilimo cha mabangayeye ni kigumu sana na hauwezi kuvuna alizeti kwa wingi, kwa sababu ya ukubwa wa mimea na pia ndege wanapenda sana bangayeye kitu ambacho kinachangia sana mavuno duni.

Ndugu zangu WATANZANIA wenzangu. Naomba niwajulishe kuwa, mafuta ya kula huku Ulaya wanatengeneza kwa kutumia zao la Canola au kwa lugha nyingine RAPESEED.

Hili zao ni rahisi sana kulima na linakubali zaidi kwenye sehemu za baridi kama Mafinga, Njombe, Tukuyu, Moshi, na Arusha.

Zao la canola huchukua miezi mitatu na nusu kuwa tayari kuvuna na ekari moja hutoa lita 700 mpaka 800 za mafuta ya kula (ALIZETI EKA MOJA UNAPATA NUSU PIPA TU LITA 100).

Ukamuaji wa mbegu zake ni rahisi sana hata kwa kutwanga na kinu tu, unapata mafuta. ni rahisi ku process (kuchakata) kama mawese tu.

Ndugu zangu, kilimo ni ajira na tusilime kama tumelazimishwa kwa kuogopa kukosa ugali. Tulime kama biashara na utajiri tunao.

Mimi binafsi huu uhaba wa mafuta nauchukua kama fursa ya kupiga hela ndefu. Mimi nitajaribu mwaka huu kulima walau ekari 50 za Canola na nitaangalia kipato nitakachopata kwa kuanzia. Najua italipa kwani zao la Canola halina gharama kulima kama mabangayeye au mahindi.

Nawakumbusha tu pia kuwa eka moja ya canola inatoa lita 800 wakati mabangayeye au mnaitaga alizeti inatoa lita 100. Hii ni mara nane zaidi.

Mafuta ya Canola pia husaidia kuweka ngozi nyororo na ni tiba kwa wenye matatizo ya joints na mifupa.

Mimi sio bwana shamba, lakini huu utafiti nimeufanya binafsi kwa kukaa na kuongea na mkulima wa Canola hapa UK (Uingereza) ambaye huwa ninanunua matrekta kwake.

Tuache kuishi kwa kukariri. Na ni aibu kwa nchi yenye ardhi kubwa yenye rutuba kuishiwa mafuta.

Uzuri wa Canola pia majani yake ni mboga na Wahehe tunaiitaga NYADUNDWE na maua yake pia unaweka kwenye mboga ukitaka.

PAMOJA NA KULIMA CANOLA, PIA TUTALETA MASHINE ZA KUTOSHA ZA KUKAMULIA MAFUTA YA KULA KWA BEI NAFUU SANA.

ASANTENI KWA KUNISOMA

KAZI NI KIPIMO CHA UTU

KC TEAM

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news