OR-TAMISEMI yasisitiza ubunifu kwa elimu bora nchini

NA ASILA TWAHA

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Gerald Mweli amesema ili Serikali iendelee kuwekeza na kupanga mipango mizuri ya elimu nchini ni lazima watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa waliopewa jukumu la usimamizi wa elimu wasimamie na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Hayo ameyasema leo Aprili 11,2022 jijini Arusha wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya maandalizi ya Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo Awamu ya Pili (EP4R) ambao lengo lake ni kuendelea kuhakikisha suala la elimu linaendelea kuwa kipaumbele nchini.

Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo Awamu ya Pili Naibu Katibu Mkuu Mweli amesema, ni pamoja ya upimaji wa mwenendo wa elimu nchini ambapo upunguza mdondoko wa wanafunzi.
Aidha, amewaelekeza wasimamizi wa elimu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi na kuongeza ubunifu wa njia za ufundishaji kwa kuhakikisha suala la usimamizi wa elimu ni kipaumbele kwa kuweka njia nzuri katika ufundishaji wa elimu kwa ujumla.

Amefafanua kuwa, Ofisi ya Rais - TAMISEMI haiwezi kusema inatekeleza majukumu yake, "bila ya kuwashukuru ninyi viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa tusimamie utendaji wetu wa kazi kwa kufanya ubunifu katika sekta ya elimu ili tutimize lengo la Serikali kwenye kuona matokeo chanya katika Sekta ya Elimu.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tunamshukuru kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri na kwa kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha suala la elimu linaendele kuwa bora nchini,"amesema Mweli.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Erick Kitali amesema, Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo Awamu ya Pili ni kutokana na upatikanaji wa takwimu sahihi suala la elimu linaendana moja kwa moja na taarifa sahihi za wanafunzi na mahitaji ya shule.

Ametoa wito kwa viongozi hao kuhakikisha wanasimamia upatikanaji sahihi kwa kutumia mifumo sahihi ili kuwezesha Serikali kupanga maendeleo mazuri ya elimu.

“Tangu 2016 mpaka sasa takwimu zetu za elimu msingi zimekuwa ni bora sana niwaombe viongozi wenzangu tuendelee na umakini katika ujazaji wa taarifa sahihi katika mfumo wa Annual School Census na SIS ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi,"amesema.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi hao katika ujazaji sahihi wa mfumo wa Madeni MIS ya walimu yasiyokuwa mishahara ili iwe ni rahisi kufanyiwa kazi kwa kuzingatia taarifa zilizo sahihi.
Awali mtoa mada ambaye ni Afisa Elimu Mkuu, Hilda Mkandawire amesema, Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo Awamu ya Pili umezingatia rasilimali watu zinaelekezwa kwenye halmshauri zenye uhitaji mkubwa ambapo amesema hii itaendelea kusaidia kutatua changamoto katika maeneo yale yanayoonekana yana changamoto kubwa ya elimu.

Aidha, mafunzo hayo yaliwashirikishwa Wakurugenzi, Makatibu Tawala Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Njombe na Wathibiti Ubora Kanda ya Kaskazini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news