Polisi waanza na mpiga chuma anayeiba pikipiki na kuua Dar

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata, Bw. Iddi Omari Ndakae (Chuma Steel) kwa tuhuma za kupora pikipiki katika maeneo ya Kigamboni na maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

"Mtuhumiwa akiwa na wenzake Aprili 16,2022 alimkodisha dereva pikipiki Jumanne Mpenja kutoka Mbagala Charambe kumpeleka Kigamboni, walipofika Visikini, Kigamboni alimpiga dereva kwa kitu kizito kichwani hadi kufariki na kuiba pikipiki yake;
Hayo yamesemwa leo Aprili 28,2022 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro wakati akizungumza jijini Dar es Salaam.

"Katika mahojiano ya kina na mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi lilibaini kuwa mtuhumiwa alishiriki katika tukio lingine la kumpiga kwa kitu kizito kichwani kisha kumuua Mkapa Nuru miaka kati ya 20 hadi 25 Agosti 27,2021 aliyekuwa mkazi wa Mbagala Kiburugwa na kumpora pikipiki.

"Baada ya kufanya tukio hilo la mauaji mtuhumiwa aliutupa mwili eneo la Visikini Dege Kigamboni ambapo katika ukaguzi wa eneo hilo kumepatikana mifupa idhaniwayo ya binadamu ambayo ni fuvu la kichwa, mifupa ya nyonga na kaptula ya jeans vyote vinavyodhaniwa kuwa ni vya marehemu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu.

"Pia amekamatwa Mfaume Donald Kapela (23) mkazi wa Kibiti sokoni ambaye alishirikiana nae na baada ya mahojiano ya kina jeshi lilifanikiwa kuipata pikipiki ya marehemu,"amesema.

Post a Comment

0 Comments