Rais Samia aliagiza Baraza la Maadili kusimamia maadili Utumishi wa Umma

NA LILIAN LUNDO-MAELEZO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameliagiza Baraza la Maadili kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kila mtumishi wa umma atambue majukumu yake na kuheshimu mipaka ya kazi yake.
Rais Samia amesema hayo leo Aprili 2, 2022, Ikulu Chamwino jijini Dodoma alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni wakiwemo wajumbe wa Baraza la Maadili.

"Hali ya utumishi wa umma sio nzuri sana, ingawa tunasifiwa kwa mabadiliko tuliyoyafanya Serikali ya Awamu ya Tano, yamekuza heshima kwenye Utumishi wa Umma, lakini heshima iliyokuzwa ni heshima ya uoga sio ya kutoka moyoni, sababu watu waliogopa kufokewa,"amefafanua Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha, Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, katika hafla fupi iliyofanyika leo Aprili 2, 2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma. 

Amesema kuwa, heshima inayotakiwa ni heshima ambayo inatoka moyoni, na mtumishi awe na itikadi ya kujitambua kama ni Mtumishi wa Umma, na pia atambue majukumu yake ni yapi, nini anatakiwa kufanya na nini hatakiwi kufanya. 

Pia amesema kuwa, kila mtumishi wa umma ni lazima aheshimu mipaka yake ya kazi, bila kuingilia mipaka ya mtumishi mwenzake ili kuzuia migogoro ndani ya ofisi za umma na kati ya kiongozi na kiongozi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Damas Daniel Ndumbaro (Mb) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika hafla fupi iliyofanyika leo Aprili 2, 2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Pindi Hazara Chana (Mb) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Jaji mstaafu Ibrahim Mipawa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo Aprili 2, 2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Peter Ilomo kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Suzan Mlawi kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo Aprili 2, 2022.

"Serikali inakwenda kuimarisha Chuo cha Utumishi pamoja na Chuo cha Uongozi ili kuweza kuwapatia mafunzo watumishi wa Umma. Baraza likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania tutakwenda vizuri,"amesema Rais Samia.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewakaribisha viongozi hao Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wowote na kwa lolote ili kushirikiana na kutoa matokea ambayo Mheshimiwa Rais anataka kuyaona kama ambavyo amekuwa akisisitiza wakati wote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Mawaziri pamoja na Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo Aprili 2,2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Daniel Ndumbaro (Mb) pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Pindi Hazara Chana mara baada ya hafla fupi iliyofanyika leo Aprili 2,2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

"Serikali na hasa Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia na shughuli za kila siku ndani ya Serikali tutawapa ushirikiano wa hali ya juu ili mtekeleze majukumu yenu," amesema Waziri Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news