TFRA yaanisha mikakati kuhakikisha wakulima wanapata mbolea

*Prof.Mshandete atoa wito kwa mwekezaji Itracom Fertilizer LTD
 
NA NURU MWASAMPETA-TFRA

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Prof. Anthony Mshandeteameweka wazimikakati mahususi ya kuhakikisha wakulima nchini wanapata mbolea bora kwa ajili ya matumizi ya kilimo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Prof. Anthony Mshandete, wajumbe wa bodi na Menejimenti ya TFRA wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi katika kiwanda cha mbolea Intracom Jijini Dodoma Victor Ngendanzi wa kwanza kushoto mbele ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania,Dkt.Stephen Ngailo.

Ameeleza mikakati hiyo Aprili 29, 2022 ambapo wajumbe wa Bodi ya TFRA pamoja na watendaji wa mamlaka hiyo walitembelea eneo kinapojengwa kiwanda hicho kwa lengo la kujionea hatua na maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kinachotarajia kuanza uzalishaji wa tani 6000 za mbolea mwezi Julai 2022.

Akieleza mikakati hiyo, Prof. Mshandete alisema mkakati wa kwanza ni kuhakisha mbolea inayozalishwa inakuwa na ubora na viwango vinavyokubalika nchini. Alisema wananchi wakiona ubora wa mbolea inayozalishwa na kiwanda hicho itakuwa rahisi kwa kiwanda kujitangaza na mbolea itauzika kiurahisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Prof. Anthony Mshandete (wa pili kulia) akihoji jambo kwa Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi katika kiwanda cha mbolea Intracom Jijini Dodoma Victor Ngendanzi walipofanya ziara kiwandani hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Akielezea mkakati wa pili Prof. Mshandete alisema ni uongozi wa kiwanda kuwa na mkakati wa mawasiliano kwa ajili ya kutangaza aina ya mbolea itakayokuwa ikizalishwa na kiwanda hicho yenye mchanganyiko wa samadi na madini mengine kama phosphate na chokaa tofauti na aina zilizozoeleka kwa wakulima nchini.

Prof. Mshandete alisema kutokana na ukweli kwamba mbolea inayozalishwa kiwandani hapo kuwa mpya kwenye soko la ndani elimu kuhusu ubora wa mbolea hiyo unapaswa kutolewa ili wananchi waweze kuifahamu na kuwa na utayari wa kuitumia na hivyo kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mbolea nchini.
Baadhi ya mitambo iliyopo kwenye kiwanda cha mbolea cha Intracom Fertilizer Limited kinachojengwa Jijini Dodoma.

Aidha, Prof. Mshandete amewataka wasimamizi wa kiwanda cha Itracom Fertilizer LTD kuwa na hari (aggressiveness) katika kutangaza bidhaa na kuwashauri kushiriki katika maadhimisho ya siku ya mbolea yanayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu ili kuwapa fursa ya kuitangaza bidhaa hiyo.

Akizungumzia suala la upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea kiwandani hapo Prof. Mshandete alisema kutatokana na namna nzuri ya kutangaza uwepo wa kiwanda hicho pamoja na kutangaza malighafi zinazotumika katika uzalishaji kutakakofanywa na mwekezaji huyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Prof. Anthony Mshandete (wa pili kulia) akiangalia na kufuatilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi katika kiwanda cha mbolea Intracom Jijini Dodoma Victor Ngendanzi katika moja ya eneo zilipo mashine walipofanya ziara kiwandani hapo tarehe 29 Aprili, 2022.

Pamoja na hayo Prof. Mshandete ametoa wito kwa mwekezaji Itracom Fertilizer LTD kutosita kuishirikisha TFRA na mamlaka nyingine za serikali pindi wanapokutana na changamoto wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza kwa upande wa mwekezaji, Dr. Ntukamazina Nepomuscene Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Itracom Fertilizer LTD alisema ujenzi wa kiwanda upo katika hatua nzuri ambapo mitambo imeshaanza kufungwa tayari kuanza uzalishaji ifikapo Julai 2022.

Aliongeza kuwa, tayari kiasi kikubwa cha samadi kimepatikana na kimefikishwa kiwandani hapo kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa mbolea hiyo.
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi inayosimamia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wakiongozwa na mwenyekiti wake Prof. Prof. Anthony Mshandete (wanne kutoka kulia) na menejimenti ya (TFRA) wakipewa maelezo na Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi katika kiwanda cha mbolea Intracom Jijini Dodoma Victor Ngen.

Uwekezaji huo utakaogharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 180 ni matokeo ya ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini Burundi na kueleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kumpata mwekezaji wa kiwanda cha Itracom Fertilizers Limited.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news