LATRA yatangaza nauli mpya za daladala na mabasi nchini

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) imetangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini.
Akitangaza kiwango hicho kipya cha nauli leo Aprili 30, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14.

Bw.Ngewe amesema nauli za daladala kuanzia kilomita 0-10 nauli itakuwa shilingi 500 kutoka sh.400 na kilomita 11-15 nauli itakuwa sh. 550 kutoka sh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa kilomita 36 hadi 40 itakuwa sh.1,100 kwa daladala tu.

Kwa upande wa nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni sh. 41.29 kwa kilomita moja kutoka sh. 36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka sh. 53.22 ambapo nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa sh.200 kwa daladala.

Post a Comment

4 Comments

  1. Nipo dodoma, bajaji kutoka mjini kwenda kikuyu wanatoza nauli 1000 badala 500 wamepandsha hivyo

    ReplyDelete
  2. Pandisha tu sio mbaya wengine tutabakia Dar es Salaam milele

    ReplyDelete
  3. Changamoto nauli hazieleweki ,,, unakuta nauli ya sumatra ni nyingine na ya wapiga debe ni nyingine,,, si kuwepo na nauli elekezi km mwenye bus akishindwa kufuata ,,, apewe adhabu mara mbili,,, haiwezekani nauli iliyotangazwa ni ndogo kuliko iliyokuwa inalipwa dar tarime

    ReplyDelete