ASKARI UHIFADHI WALIODANGANYA KUVUNA MAMBA BUCHOSA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemuelekeza Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii kuwachukulia hatua za kinidhamu Askari wa Uhifadhi watakaothibitika kuidanganya Serikali kwamba wameshiriki katika zoezi la kuvuna mamba wawili Wilayani Buchosa mkoani Mwanza.
Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric James Shigongo kuhusu mikakati ya Serikali ya kuzuia mamba wanaoua watu Jimboni Buchosa.

Amefafanua kuwa Serikali katika kukabiliana na changamoto hizo, inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Migongano baina ya Binadamu na Wanyama wakali na waharibifu.
Awali akijibu swali la msingi Mhe. Masanja alisema kuwa Serikali imevuna jumla ya mamba wawili katika wilaya hiyo.

“Kuanzia kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 jumla ya mamba wawili wamevunwa Wilaya ya Buchosa,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news