FIFA yatupilia mbali rufaa ya Algeria dhidi ya Cameroon

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limetupilia mbali shauri la timu ya Taifa ya Algeria la kutaka mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon urudiwe.
FIFA imesema imefunga mafaili ya shauri hilo, hivyo Cameroon itashiriki Kombe la Dunia bila kikwazo huko nchini Qatar.

Tangazo hilo limetolewa Jumamosi ya Mei 7,2022 na shirikisho hilo.Machi 29,2022 Cameroon ilishinda ugenini 2-1 dhidi ya Algeria na kufuzu kwa bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza Algeria kushinda ugenini bao 1-0.

Aidha, Machi 31, Shirikisho la Soka la Algeria lilitangaza kukata rufaa kwa FIFA kuomba mechi hiyo irudiwe kwa sababu ya kile walichoelezea kuwa refa wa Gambia, Bakary Gassama alichezesha mechi ya aibu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, kamati ya waamuzi wa FIFA ilikataa kukubali ombi hilo. Kuondolewa kwa Algeria kulionekana kama janga la kitaifa. Baadaye wafuasi wa timu hiyo waliandamana mara kadhaa mbele ya makao makuu ya FIFA huko Zurich, Uswizi.

Kwa uamuzi huo,timu za Cameroon, Ghana, Morocco, Senegal na Tunisia ambazo zilifuzu kutoka ukanda wa Afrika kucheza fainali za Kombe la Dunia muda ukifika watakutana na wenzao huko nchini Qatar mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news