Katibu Mkuu Dkt.Jingu:Jamii ipewe elimu kuhusu Anwani za Makazi

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt.John Jingu amezitaka halmashauri kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa Anwani za Makazi na Postikodi katika maeneo yao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Dkt. John Jingu akikagua moja ya nguzo za barabarani na mbawa iliyowekwa katika eneo la Katumba kuonesha Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Rugwe jijini Mbeya wakati wa ziara yake kujionea maendeleo ya zoezi hilo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na Kyela kwa nyakati tofauti alipofanya ziara yake ya kujionea maendeleo ya utekelezaji wa zoezi hilo Mei 18,2022 jijini Mbeya.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu akisoma mbawa za barabarani zitakazo tumika katika zoezi la Anwani za Makazi alipotembelea Karakana ya Kisemile Sign Artist iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rugwe Jijini Mbeya wakati wa ziara yake kujionea maendeleo ya zoezi hilo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu akikagua Nguzo za barabarani na Mbawa zitakazo tumika katika zoezi la Anwani za Makazi katika Karakana ya Kisemile Sign Artist iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rugwe Jijini Mbeya wakati wa ziara yake kujionea maendeleo ya zoezi hilo.
Alieleza kuwa jamii inapaswa kupewa elimu ya umuhimu wa masuala ya anwani za makazi ili kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuhakikisha kila mmoja analibeba kwa uzito unaotakiwa.

“Endeleeni kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa anwani za makazi katika maeneo yenu, kwa kuzingatia faida zake ikiwemo kurahisisha shughuli za maendeleo,”amesema Dkt.John Jingu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa wakiangalia vibao vya namba za nyumba kwa ajili ya zoezi la anwani za makazi wakati wa ziara yake katika Wilaya hiyo Jijini Mbeya. 

Aliongezea kuwa, ili kutatua changamoto za uelewa mdogo kwa jamii, aliwataka viongozi wa halmashauri kushiriki kikamilifu kwa kubuni mbinu mbalimbali zinazoendana na mazingira husika huku akiwataka kuendelea kuvitumia vyombo vya habari katika utoaji wa elimu hiyo.

“Hakikisheni mnavitumia vyombo vya habari vilivyopo katika jamii zetu ili kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja huku mkifanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha zoezi la Anwani za makazi linakamilika kwa wakati uliokusudiwa,”amesema Dkt. Jingu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu pamoja na timu aliyoongozana nayo wakiangalia vibao vya namba za nyumba katika Karakana ya Ibililo kwa ajili ya matumizi ya anwani za makazi Wilaya ya Rugwe Mbeya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt. Vicent Anney aliahidi kuendelea kusimamia zoezi hilo ili kuendelea kuunga mkono jutihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika adhima yake ya kuiletea nchi maendeleo.

“Wilaya yetu imejipanga vizuri kusimamia zoezi la anwani za makazi, tunaahidi kutomuangusha Mhe. Rais wetu kwa kuendelea kutoa elimu kwa jitihada ili kila mwananchi aone umuhimu wa zoezi hili,”amesisitiza Dkt.Anney.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu akiangalia vibao vya namba za nyumba vilivyovyoandaliwa kwaajili ya zoezi la anwani za makazi Wilaya ya Kyela Jijini Mbeya.

Aliongezea kuwa zoezi likikamilika litarahisisha utekelezaji wa majukumu ya kiutawala katika ufuatiliaji na kujua taarifa za wananchi ambazo zitasaidia katika matukio mbalimbali yanapotokea.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya anwani za makazi kwa Wilaya Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo Bw. Castory Makeule alisema Halmashauri imejipanga vyema ili kuhakikisha elimu inayafikia makundi yote yanayohusika na kurahisisha utekelezaji wake.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu akioneshwa moja ya kibao cha anwani ya taasisi wakati wa zoezi la kukagua shughili za utekelezaji Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Jijini Mbeya.

“Zoezi la ugawaji wa namba katika kata zote 29 limekamilika ikiwa ni sambamba na zoezi la uingizaji wa taarifa katika mfumo wa makisio ya taarifa 65,500 ambapo mpaka sasa jumla ya taarifa 67,685 zimeingizwa kwenye mfumo sawa na asilimia 101.77,”amesema Makeule.

Aidha, halmashauri imeweza kuandaa nguzo/vibao 1000 zitakazowekwa katika barabara ndani ya Halmashauri ambapo kazi ipo katika hatua za mwisho ya ukamilishaji upakaji wa rangi na uandikaji wa majina ya mitaa na barabara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news