🔴LIVE:Rais Samia akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani jijini Arusha

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Sheria za Habari ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kubinya uhuru vya vyombo vya habari zirekebishwe.

Rais Samia ameyasema hayo leo Mei 3 ,2022 wakati akiwahutubia Wadau wa Vyombo vya Habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' katika ukumbi wa Gran Melia Hotel jijini Arusha.

“Nimeelekeza Sheria zirekebishwe lakini kwa majadiliano pande zote na sit u kwamba sisi tunataka nini. Nimemwelekeza Waziri sheria za habari zirekebishwe kwa kushirikisha wadau wote,”amesema Rais Samia.

Rais Samia pia ameshauri waandishi wa habari kuwa Wazalendo kwa kuandika mambo mazuri za kutetea Bara la Afrika huku akiwataka waandishi wa habari kuzitangaza mila na desturi nzuri za Tanzania.

“Tunazo mila na desturi tunapaswa kuzilinda, na nyinyi waandishi wa habari mnatakiwa kuzilinda ili kuepuka mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu. Baadhi ya watu wanaposti picha chafu mtandaoni, wanajianika mtandaoni, wengine wanafanya hivyo kwa kutojua madhara ya kufanya hivyo. Wa kwenda kuzionesha changamoto za kidigitali,"amesema Rais Samia.

Naye Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiaa Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwa kipindi kifupi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news