Mahakama yaridhia wabunge 19 waliovuliwa uanachama CHADEMA kuendelea na shughuli za kibunge

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesema wabunge 19 waliovuliwa uanachama na CHADEMA, waendelee kufanya shughuli zao za kibunge hadi Mahakama itakaposikiliza maombi yao ya zuio la muda kuhusu ubunge wao.

Uamuzi huo umetolewa leo Mei 16, 2022 na Jaji John Mgeta baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Wabunge hao waendelee kuwa Bungeni ama lah, ambapo Juni 13, 2022 ndio atasikiliza zuio hilo.

Hivi karibuni Kamati Kuu ya CHADEMA imepiga kura na kuwafukuza wanachama hao 19 waliokuwa wanatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu kwa kosa la kuapishwa kuwa wabunge bila ruhusa ya chama chao.

Kikao hicho ambacho kilichukua muda mrefu baada ya mkutano wa Baraza Kuu uliofanyika Mlimani City Dar es Salaam, kiliisha kwa kura za Matokeo ya jumla ya Idadi ya wajumbe 423, Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%, Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%, na wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%.
Wanawake wa Chadema Bawacha waliofukuzwa ni makada waliokuwa mstari wa mbele kukipigania chama hicho na baada ya Bazara Kuu kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza ndani ya chama kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge kinyume cha matakwa ya chama hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news