Mheshimiwa Neema Lugangira awapongeza wabunifu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela

NA LORIETHA LAURENCE, NM-AIST

MBUNGE wa Viti Maalum Asasi za Kiraia na Mashirika yasio ya Kiserikali,Mhe. Neema Lugangira ametoa kongole kwa wabunifu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kuzalisha bidhaa za kuimarisha lishe.
Mbunge wa Viti Maalum Asasi za Kiraia na Mashirika yasio ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira (Kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Kilimo, Sayansi ya Chakula na Usalama wa Lishe (CREATES-FNS) Bibi. Rose Mosha akielezea kuhusu bidhaa za Nutrano, Omega 3 na Super Grow wakati alipotembelea banda la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu tarehe 19 Mei, 2022 jijini Dodoma.

Ametoa pongezi hizo Mei 19, 2022 alipotembelea banda la taasisi hiyo uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania ambapo alipata maelezo kuhusu bidhaa za Nutrano na Omega 3 zinazaotatua matatizo ya utapiamlo: Buheri wa Afya inayotatua magonjwa nyemelezi na Super Grow chakula cha Samaki.

“bidhaa ni nzuri na zimejikita zaidi katika kuimarisha lishe ,natamani bidhaa hizi zingawafikia walengwa hususani mikoa ambayo imeadhiriwa na utapiamlo,” amesema Mhe.Neema.Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (Kushoto) akipata maelezo kuhusu ugali Cooker ubunifu uliofanywa na Mwanafunzi wa Shahada ya Umahili kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi. Tuse Mwasambili (kulia) alipotembelea banda la Chuo hicho tarehe 19 Mei, 2022 jijini Dodoma.

Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Kilimo, Sayansi ya Chakula na Usalama wa Lishe (CREATES-FNS) kilichopo chini ya taasisi hiyo Bibi. Rose Mosha ameahidi kufanyia kazi ushauri huo ili kuwafikia walengwa wengi zaidi.

Bibi. Rose alieleza kuwa bidhaa hizo zimefanyiwa tafiti na wanafunzi wa NM-AIST waliofadhiliwa masomo yao na kituo hicho ikiwa ni kusimamia kauli mbiu ya Elimu kwa Jamii na Viwanda ( Academia for Society and Industry) kwa kuangalia changamoto zinazoikabili jamii na kuzifanyia tafiti kisha kutoa suluhisho.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete (kulia) akiangalia bidhaa ya Uji Tayari wenye Virutubisho (Instant Porridge) ulioandaliwa na Bi. Rufina Fredrick wakati wa maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania tarehe 19 Mei,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Ndg. Waziri Salum (Kulia) akimsikiliza Mbunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi. Philipina Shayo katika maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania tarehe 19 Mei, 2022 Dodoma.

Naye Mkurugenzi wa Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bw. Waziri Salum amewataka wabunifu hao kutumia fursa ya kuomba ufadhili kupitia programu za ufadhili unaotolewa na Mamlaka hiyo ili kuzifanya bunifu hizo kwenda mbele zaidi.

“tumie fursa ya kuomba ufadhili kupitia programu za ufadhili zinazotolewa na ofisi za TEA ambazo hutangazwa kupitia tovuti ya mamlaka hiyo ili kuendeleza bunifu zenu, alisema Mkurungezi wa Miradi,Waziri.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete (mwenye koti la kijivu) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wanafunzi walioshiriki maonyesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania tarehe 19 Mei,2022 jijini Dodoma. (Picha na Lorietha Laurence,NM-AIST).

Ameongeza kuwa , baadhi ya wabunifu ni wanufaika wa ufadhili huo akiwemo Mbunifi wa Chujio la Maji la Nanofilter Profesa Askwar Hilonga ambaye mara kwa mara amekuwa akipata ufadhili kupitia ubunifu wake huo uliosaidia jamii ya watu wa Arusha kupambana na magonjwa ya tumbo pamoja na kutoa ajira kwa wanawake na vijana 130.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi ya Nelson Mandela imefanikiwa kuleta wabunifu 18 wakiwa na bunifu mbalimbali ikiwemo Ugali Cooker, Mfumo wa kumsaidia mtu asiyeweza kuona, bidhaa za Tunda la Kweme, unga wa virutubisho, chujio la maji la nanofilter, mfumo wa kuchuja maji taka, buheri wa afya, Nutrano , Omega na nyinginezo nyingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news