NAIBU WAZIRI KIKWETE AWATAKA WATENDAJI WA WIZARA YAKE KUENDELEA KUTOA HUDUMA KARIBU NA WANANCHI

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa wizara yake kuendelea kutoa huduma karibu zaidi na wananchi.
Kikwete amesema hayo wakati alipo tembelea banda la Wizara yake katika Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi jijini Dodoma ambapo Wizara yake ilikuwa inatoa huduma papo hapo.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilishiriki katika Maonesho hayo ambayo yamefanyika kuanzia tarehe 23 hadi 30 Aprili 2022 katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion Center jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments