Ni Royal Tour kesho jijini Zanzibar, viongozi waeleza makubwa, wananchi waanza kusherehekea mafanikio

 NA DIRAMAKINI

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa kwa wingi katika Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour utakaofanyika visiwani Zanzibar kesho Aprili 7, 2022.
Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na baadhi ya viongozi na viongozi wastaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wakifafanua kuhusu faida za Royal Tour katika uchumi wa Zanzibar, Uwekezaji, na kuongeza fursa za ajira kwa vijana, wafanya biashara na wajasiriamali waliojiajiri kupitia sekta ya utalii visiwani humo.

Uzinduzi wa Filamu hiyo utafanyika Jumamosi hii Mei 7, 2022 ambapo wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi Hoteli ya Golden Tulip jirani na Uwanja wa Ndege kumpokea na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio yanayoanza kuonekana baada ya uzinduzi wa filamu hiyo nchini Marekani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mstaafu, Balozi Seif Ali Iddi amesema, Royal Tour itasaidia kuitambulisha Tanzania kuwa ipo Afrika Mashariki na inaweza kuwakaribisha Watalii wengi kuja kufanya shughuli za Utalii.

Amesema, Watanzania wajitokeze kwa wingi kuitaza Filamu hiyo ili kuona filamu hiyo Aprili 7, mwaka huu. Huku pia akipongeza juhudi kubwa zinazofamywa na Dkt. Husein Mwinyi na Rais Samia za kuwaletea maendeleo wananchi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salumu amepongeza pia juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Husein Mwinyi kwa kazi nzuri wanazofanya kuiweka Tanzania kwenye sura ya dunia katika masuala ya uchumi na uwekezaji.

"Tunakwenda kuzindua Royal Tour ambapo tunategemea utekelezaji wake utasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji na utalii ambao ni kiungo kwa uchumi wa Zanzibar na tunawakaribisha sana wananchi wote kushiriki pale Golden Tulip na kufuatilia kwenye vyombo vyetu vya habari tuone, kwa sababu tunajua kila mwananchi ana nafasi ya kuitangaza Tanzania," amesema Dkt.Mkuya.
"Royal Tour malengo yake ni makubwa sana pamoja na mambo mengine wakati tunashiriki katika vikao Washington tumeona jinsi gani mbali ya Serikali, lakini pia wafanyabiashara wa pande zote mbili yaani Marekani na Tanzania wamesaini mikataba mbalimbali,"amesema.
Neema ya Royal Tour yasherehesha sikukuu ya Idi pili Zanzibar baada ya watu wa kada mbalimbali visiwani humo kuonesha furaha waliyo nayo juu ya uzinduzi wa filamu hiyo. 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Royal Tour itakuza utalii visiwani humo na kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wajasiriamali wa sekta ya utalii.  
Huku wakiahidi kushiriki kikamilifu kwenye uzinduzi wa filamu hiyo utakaofanyika visiwani humo katika Hoteli ya Golden Tulip siku ya Jumosi Mei 7,2022.

Post a Comment

0 Comments