Sekondari za Pera na Msata zapewa marumaru kutoka Keda (T) Ceramics Co.Ltd

NA DIRAMAKINI

SHULE za Sekondari za Pera na Msata zimapewa marumaru zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 na Kiwanda cha kutengeneza Marumaru cha Keda (T) Ceramics Co. Ltd.

Akizungumza mara baada ya zoezi la kukabidhi Marumaru hizo kwenye shule ya Sekondari ya Pera Ofisa Tawala wa kiwanda hicho, George Lulandala amesema kiwanda hicho kitaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na changamoto za sekta ya elimu.
Lulandala amesema kuwa Maramaru hizo ni kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya usomaji kwa wanafunzi.

"Vifaa hivi tunatoa ikiwa ni sehemu ya kurudisha mchango kwa jamii tutaendelea kushiriki shughuli za wananchi ili kuwaleteamaendeleo,"amesema Lulandala.

Aidha, amesema wameamua kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani ameonyesha kuwajali wananchi wakiwemo wanafunzi ambapo amefanya mambo mengi kwenye sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa na miundombinu.

Ameongeza kuwa Sekondari ya Msata imepatiwa maboksi 203 huku Pera Sekondari wakipata maboksi 100 na bado tutaendelea kutoa misaada mbalimbali ili kuhakikisha kuboresha sekta mbalimbali.

"Kwa kipindi cha nyuma tumesaidia kituo cha afya cha Pera na huduma mbalimbali kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali kwenye wilaya na mkoa,"amesema Lulandala.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Iddi Ng'oka amesema kuwa wanashukuru kiwanda hicho kwa msaada walioutoa kwani bila ya kuweka Marumaru sakafu imekuwa ikiharibika mara kwa mara.

Ng'oka amesema kuwa wanaomba wapewe tena maramaru kwani kuna baadhi ya madarasa hayana Marumaru pamoja na ofisi hivyo wakipatiwa nyingine itasaidia sana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news