Uongozi wa Rais Samia utasimamia misingi ya haki, demokrasia na utawala bora-Shaka

*Awahimiza watanzania kuunga mkono jududi za Serikali za kuleta maendeleo

NA SAID MWISHEHE

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ameendelea kuhimiza wananchi wote kuhakikisha wanashirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo na uongozi wa Rais umekuwa kinara katika kutenda haki, demokrasia na utawala bora.
Wanachama wa CCM mjini Babati wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani.

Aidha amesema tangu Rais Samia ameingia madarakani amekuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo huku akiwataka wananchi na shaka yoyote kwani Rais atawavusha salama na ataendelea kuwatumikia kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo mkubwa.

Akizungumza kwenye mikutano yake aliyofanya mkoani Manyara kwa nyakati tofauti Shaka amesema uongozi wa Rais Samia pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo umekwenda kufungua uhuru, haki na demokrasia kwa kila mmoja wetu na lengo ni kuhakikisha wananchi wanashiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa la Tanzania.
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza kwenye moja ya mikutano yake ya ndani mjini Babati,mkoani Manyara akiwa kwenye ziara yake ya kujitambulisha mbele ya wanachama wa ccm , kama mlezi mpya wa chama hicho akichukua nafasi ya Waziri mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda.

“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara katika kuheshimu misingi yakutenda haki, demokrasia na utawala bora na tangu alipoingia madarakani ameweka mazingira mazuri ya kufanya siasa hapa nchini.

Shaka amesema wananchi hivi sasa ni mashahidi wameshuhudia vyama vya siasa na wanasiasa wakiwa huru kufanya shughuli zao za kisiasa bila kusumbuliwa tofauti na huko nyuma.“Rais Samia ametoa uhuru mkubwa kwa wanasiasa na vyama vya siasa kufanya siasa kiungwana na kuvumiliana” amesema Shaka na kuongeza

“Rais Samia tangu aingie madarakani ameshakutana mara mbili na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe lakini pamoja viongozi wengine wa upinzani.Tunaposema Rais Samia amekuwa kinara wa haki, kinara wa demokrasia na kinara wa utawala bora tunayo mifano.

“Ndio maana husikii wanasiasa wakilalamika lakini hata yale mambo ya kusikia fulani kapotea , haonekani siku hizi hayapo tena.Watu wako huru kufanya shughuli zao na wala hawasumbuli, Rais Samia nia yake ni njema kwa taifa hili hivyo ni wajibu wetu kumuunga mkono na kumpa ushirikiano.”amesema Shaka.
Wanachama wa CCM mjini Babati wakifurahia jambo baada ya kumsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani. (PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG).

Pamoja na hayo Shaka amewataka wananchi wote ujumla kujiandaa kwa mambo makubwa zaidi ya kufurahisha ndani ya utawala wa Rais Samia na kwa uthubutu ambao amekuwa akiuonesha ni imani yake yajayo yanafurahisha zaidi.

Hata hivyo, katika ziara yake kwenye mkoa huo, Shaka ameendelea kuwakumbusha wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanaelezea mafanikikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao kotokana na fedha wanazopewa na Serikali badala ya kukaa kimya wakati kuna mambo makubwa ya maendeleo yamefanyika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news