Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Mei 13, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Pula ya Botswana inanunuliwa kwa shilingi 185.11 na kuuzwa kwa shilingi 188.32 huku Dola ya Canada (CAD) ikinunuliwa kwa shilingi 1754.5 na kuuzwa kwa shilingi 1771.5.
Pula ya Botswana. (Picha na Depositphotos).

Dola ya Zimbabwe (ZWD) inanunuliwa kwa shilingi 0.43 na kuuzwa kwa shilingi 0.44 huku Shilingi ya Uganda (UGX) ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 13,2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.7 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2378.01 na kuuzwa kwa shilingi 2402.02.

Kwa mujibu wa BoT, Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Franka ya Rwanda (RWF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.27.
Aidha, Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2288.1 na kuuzwa kwa shilingi 2299.5 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 140.8 na kuuzwa kwa shilingi 142.1.

Kwa upande wa Kwacha ya Zambia (ZMK) inanunuliwa kwa shilingi 132.8 na kuuzwa kwa shilingi 135.1 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.08 na kuuzwa kwa shilingi 50.53.

Post a Comment

0 Comments