Waziri Bashungwa awashirikisha wadau hitaji la Machinga nchini

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Sekta za kifedha na taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa huduma za mikopo ya gharama nafuu kwa ajili ya kukuza biashara za wajasiriamali wadogo.
Akifungua kongamano la Jukwaa la Maendeleo ya Sekta ya Fedha jana Mei 20, 2022 jijini Dodoma Mhe. Bashungwa ameziomba taasisi kuinua kundi hilo kwa lengo kwa kutoa mikopo ili kuboresha mazingira ya biashara na kuinua wigo wa ulipaji kodi.

Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira ya kutambua Wamachinga kuwa Sekta rasmi na kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara

Amewahakikishia wajasiriamali wadogo (wamachinga) wote nchini kuwa Serikali ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha inatengeneza mazingira wezeshi kwa ajili yako kote nchini hivyo Wizara husika zitahakikisha zinatekeleza kwa weledi dhamira ya Rais Samia ya kuleta maisha bora kwa machinga inafanikiwa.

Aidha, amewaagiza Makatibu wa Wizara ya fedha, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsi, wazee na mahitaji Maalum na Ofisi ya Rais TAMISEMI kukaa kwa pamoja ili kujadili na kuchambua maazimio ya kongamano hilo na kupata muelekeo wa Sekta ya Machinga nchini.

Bashungwa amesema Sekta ya Machinga ina fursa kubwa katika kuchangia uchumi wa nchi hivyo amewataka viongozi mbalimbali kuhakikisha wanatumia kongamano hilo kujadili kwa kina maeneo yaliyofanywa vizuri katika sekta hiyo, changamaoto zilizopo na fursa za kiuchumi ambazo zikisimamiawa ipasavyo zitaleta mafanikio katika sekta ya Machinga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news