Ajali ya treni yaua, yajeruhi zaidi ya 100 mkoani Tabora

NA DIRAMAKINI

WATU kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea mkoani Tabora hadi Dar es Salaam kuanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC),Bi. Jamila Mbarouk amesema kuwa kuwa, ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 22,2022 majira ya saa tano asubuhi.

Amesema,treni hiyo namba Y 14 yenye injini namba 9019, ikiwa na mabehewa nane yaliyobeba abiria 930 iliipofika eneo la Malolo (Kilomita 10 kutoka stesheni ya Tabora) mabehewa matano ya abiria daraja la tatu, behewa moja la vifurushi, behewa moja la huduma ya chakula na vinywaji na behewa la breki yalianguka na kusababisha ajali.
Bi. Jamila amesema, ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanne wakiwemo watoto wawili, wa kike mwenye umri wa miaka mitano na wa kiume miezi minne na watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke.

Amesema, kuna majeruhi 132 ambapo tayari wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Kitete -Tabora kwa ajili ya matibabu na wanaendelea vizuri.
Amesema, shirika linaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali kutoka Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es Salaam huku likiendelea kufuatilia kwa karibu, kufahamu chanzo cha ajali ili kuchukua hatua. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news