Ashura Athuman:Mimi nimejiandaa kuhesabiwa na familia yangu,bila kujali mwanangu Aisha ana ulemavu wa miguu, naye nitahakikisha anahesabiwa ili awe sehemu ya Watanzania ambao watajumuishwa katika mipango ya maendeleo ya Taifa

"Mimi nimejiandaa kuhesabiwa na familia yangu,bila kujali mwanangu Aisha ana ulemavu wa miguu, naye nitahakikisha kwamba, anahesabiwa ili awe sehemu ya Watanzania ambao watajumuishwa katika mipango ya maendeleo ya Taifa. Ndugu mwandishi, katika jamii ninayotoka kuna imani imani fulani ambazo huwa hazina mrengo mwema katika jitihada za namna hii, lakini ninaamini kwa haamsa ambayo inaendelea kufanywa na Serikali kila mmoja ataondoa dhana potofu na kuwa wa kwanza kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23,"amesema Bi.Ashura Athuman mkazi wa Mbagala Charambe katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam wakati wa mahojiano na DIRAMAKINI.

Post a Comment

0 Comments