Azam kuvusha abiria kutoka Magogoni kwenda Kigamboni

NA DIRAMAKINI

WAKALA wa Ufundi na Umeme Tanzania (TAMESA) imefikia makubaliano na kampuni ya Azam Marine ya kuvusha abiria kutoka Magogoni kwenda Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 13, 2022 na Kitengo cha Masoko na Uhusiano TAMESA imeeleza kuwa, imefikia makubaliano na kampuni hiyo wakati wakiendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake.

Hatua hiyo inafikiwa baada ya siku za hivi karibuni wananchi wanaokaa Kigamboni na vitongoji vyake kupata adha ya usafiri baada ya kivuko cha MV Magogoni kuharibika na kushindwa kufanya safari zake kama ilivyo kawaida.

Aidha,hali hiyo ilisababisha kivuko cha MV Kigamboni kuelemewa na abiria walikuwa wakivuka kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili, huku wakijazana, ambapo magari yalizuiliwa kuvuka kutokana na kivuko hicho kuwa kidogo.

Wakati huo huo, kupitia taarifa hiyo TAMESA imewashauri wananchi kuacha kutumia mitumbwi ili kulinda usalama wao katika eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news