Dirisha la usajili Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite msimu wa 2022/2023 kufunguliwa Julai 1

NA DIRAMAKINI

DIRISHA la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite msimu wa 2022/2023 litafunguliwa Julai 1, 2022 na kufungwa Agosti 31, 2022.
Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo.

Katika kipindi hicho Klabu zinatakiwa kukamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa.

Klabu zote zinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha kufungwa. Yeyote atakayekutana a changamoto awasiliane na Idara ya Mashindano TFF.

Aidha Dirisha Dogo lenyewe litafunguliwa Desemba 16, 2022 na kufungwa Januari 15, 2023;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news