Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya Mwaka 2022 na Sensa zilizopita Tanzania

NA DIRAMAKINI

SENSA ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi, viwango vyao vya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo, hali ya makazi na taarifa nyingine.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika sensa ya mwaka 2022 inatarajiwa kuwa na vitu vipya kama vile;

>Kutenga maeneo ya kijiografia ya kuhesabia watu katika ngazi za kitongoji/mtaa na upatikanaji wa taarifa za kitakwimu katika ngazi za kitongoji/mtaa pamoja na kuwa na mipaka ya kudumu katika ngazi hizo;

>Matumizi ya Vishikwambi (tablets) katika hatua zote za utekelezaji wa sensa kwa lengo la kupunguza gharama;

>Nyongeza ya maswali yatakayowezesha upatikanaji wa taarifa zaidi za kitakwimu ikilinganishwa na Sensa ya Mwaka 2012:-

1:Taarifa za kidemografia (umri wakati wa ndoa ya kwanza);

2:Maswali yanayohusu ulemavu (Kichwa kikubwa, Mgongo wazi, Kifafa/Epilepsy, Mbalanga/storiasis na Usonji/autism);

3:Maswali ya uhamaji kulingana na mapendekezo ya IOM (International Organization of Migration);

4:Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho NIDA, vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo, Mzanzibari mkazi, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva);

5:Maboresho ya maswali ya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na idadi ya kaya ziliko kwenye sekta isiyo rasmi;

Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA

>Takwimu za nyumba (orodha, hali ya umiliki na aina ya nyumba)

>Maswali ya kilimo na mifugo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news