Maneno yaliyowapa faraja, nguvu wadau wa habari nchini kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

"Sina tatizo, naona muwe na 'regulator', bodi yenu moja, ili mmoja wenu akienda kinyume na maadili (ya uandishi wa habari), mnamshughulikia nyinyi wenyewe.Nipo nanyi na Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) katika hatua ya kuelekea mabadiliko ya sheria za habari,"amesema Mhe.Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo Juni 13,2022, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma alipokutana na wadau wa habari nchini.
Wadau wa habari akiwemo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Anita Mendoza, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEF, James Marenga, Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN na Angela Akilimali, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe.Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (anayenakili jambo) ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe.Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (AG) kulia akizungumza na wadau wa habari waliomtembelea ofisini kwake bungeni jijini Dodoma leo.
Angela Akilimali, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), akimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe.Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi wakati akizungumza na wadau wa habari ofisini kwake bungeni, jijini Dodoma leo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe.Jaji Dkt.Eliezer Mbuki Feleshi (AG) akiangalia nakala ya marekebisho ya sheria aliyokabidhiwa na Deodatus Balile (kushoto), Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), jijini Dodoma wakati TEF na wadau wengine wa habari walipokuwenda kumtembelea AG Feleshi.
Wadau wa habari akiwemo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile,James Marenga, Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN na Angela Akilimali, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe.Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (anayenakili jambo) ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments