Mkutano wa Tathmini ya Msimu wa Ligi ya NBC 2021/2022 na Maboresho katika Sekta ya Mpira wa Miguu chini ya Serikali ya Awamu ya Sita watoa mwelekeo chanya

NA DIRAMAKINI

LEO JUNI 30, 2022 WATCH TANZANIA IMERATIBU MKUTANO MAALUM NA MUHIMU ULIOANGAZIA TATHIMINI YA MSIMU WA LIGI KUU YA NBC NA MABORESHO KATIKA SEKTA YA MPIRA WA MIGUU CHINI YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA MWAKA 2021-2022, ufuatao ni mfululizo wa maelekezo ya washiriki;

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO NA SANAA PAULINE GEKUL

"Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa karibu sana na sekta yetu ya michezo ndio maana mwaka jana aliagiza kuwekwa nyasi bandia kwenye viwanja vyetu na kupungua kodi ya uingiza wake hapa nchini;
"Ndani ya hii bajeti mpya tunakwenda kuboresha viwanja saba vya mpira hapa nchini na kupunguza bei ya vifaa vya michezo kutoa hamasa kwa vijana wetu".

ALMAS KASONGO

"Wachezaji wa nje wanaotakiwa kuja nchi kushiriki ligi kuu ya Tanzania wanatakiwa kusajiliwa na vilabu vyao ( awe katika timu ya taifa na awe amecheza mechi angalau asilimia 70 za timu ya Taifa) na kama sio timu ya Taifa basi atoke nchi ambayo ipo katika 20 bora katika ranking ya FIFA Afrika "
"Katika timu 16 zinazoshiriki ligi kuu ya NBC Tanzania ni timu 12 tu zinawachezaji toka nje au wakigeni hii nikuifanya timu kuongeza bidii uwanjani na kujitangaza kutipitia wachezaji wale".

ANTHONY MTAKA

"Ifike hatua tusikwepe matukizi ya teknologia hii tabia ya kuweka matumani yote kwa binadamu marefa sio sawa, kama tunaweza fanya marekebisho ya viwanja na kuleta wachezaji wa gharama basi pia tutumie teknologia kuongeza ufanisi kwenye ligi yetu"
"Tanzania bado tunakaulimbiu za kienyeji kama michezo ni Afya, michezo ni burudani na upendo ifike hatua tubadirike kauli hizi tuzifute kwani karne hii Michezo ni biashara, Ni ajira na ni fursa ya kuondoa umasikini kwenye familia zetu " 

ISMAIL RAGE

"Kanuni inasema mwenye mpira duniani ni FIFA, Afrika ni CAF na Tanzania ni TFF hivyo tuache ushabiki usio na maana pale Mwekezaji akijitokeza kudhamini ligi yetu kusudi ipande thamani, mfano mzuri firigisu alizofanyiwa GSM kipindi anataka kudhamini ligi hii sio sawa"
"Vilabu vyetu vitambue kwamba kuwa bingwa Tanzania peke yake isiwe kigezo cha kuvimba kichwa na kujiona wewe bora zaidi, utakuwa bora zaidi endapo utashindana na wakubwa wenzio huko duniani na kuwashinda " 

GODWIN SEMUNYU

"NBC iliyoingia kudhamini ligi kuu tulikuwa na malengo ya kibiashara ambayo ni ya muda mrefu na kusaidia jamii kama sehem ya kurudisha shukrani kwa jamii yetu"
"Sisi ndio wanadhamini pekee tulioanza kutoa bima kwa wachezaji, hii inamaanisha sisi tumechukulia michezo kwa vijana ni Ajira hivyo Bima kwake ni kitu cha msingi sana na itamsaidia mchezaji pale atakapopata changamoto ndani ya ajira yake" 

ALLY MAYAY 

"Sheria namba moja kwenye sheria 17 za mchezo wa soka inazungumzia miundombinu hivyo hii ni kitu cha kwanza kabisa kufanyiwa marekobisho kwenye soka letu lipande dhamini "
"Napenda kuipongeza sana serikali kuweza kuweka mifumo mizuri kuinua soka letu hapa nchini ikiwemo kupunguza tozo kwenye nyasi bandia na pia tozo zinazopatikana kwenye michezo ya kubahatisha( betting) ziende kuboresha michezo nchini"

HASSANI BUMBULI

"Ligi yetu ya msimu huu imekuwa bora sana kwa sababu mambo mengi yameimarishwa na kufanyiwa kazi, serikali yetu pedwa imeweza kuingilia katika na kuweka mambo sawa ikiwemo kuweka mifumo rafiki katika kuboresha miundombinu " 
AHMED ALLY

"Simba tulichelewa kufanya mabadiliko ya timu kutoka msimu uliopita kwenda msimu ujao hii ni sababu kuu ya Simba kusuasua msimu huu, hata kama msimu huu ingeshinda ubingwa basi msimu ujao ingefeli kushinda ubingwa. Tulichelewa kufanya mabadiliko kutoka msimu wa nne kwenda msimu wa tano"ahmed
"Lazima tukiri bado tuna changamoto kubwa ya viwanja, CEO wa Bodi ya Ligi yupo hapa. Muda mwingine ukiwa unauangalia uwanja kwa juu juu utaona uko vizuri lakini ukicheza unakuta ni mbovu" 

MONALISA

"Miaka ya nyuma ilikuwa ngumu sana kuwakuta watoto wa kike viwanjani lakini Leo hii katika idadi kubwa ya washabiki wanaojaza uwanja kushabikia timu zao wanawake pia wamo, hii ni kutokana na hamasa nzuri kutoka kwa wasanii na viongozi wao"
"Naomba niiombe bodi ya ligi ya Tanzania kuona ni kwa namna gani wanaweza kutumia wasanii kutangaza zaidi ligi yetu na kuongeza ushabiki sio tu wa simba na yanga bali hata kwa timu zingine kuongeza idadi ya wafuasi"

PRISCA KISHAMBA

"Moja ya kasoro kubwa kwangu kama mwandishi nimeiona kwenye ligi kuu msimu huu wa 2021-2022 ni ile ya udhamini wa kampuni ya GSM, ilikuwa ni kasoro ambayo ilionesha bodi ya ligi haikuwa huru kama ambavyo tumekuwa tukiambiwa " 
"Natamani kuona msimu ujao vilabu vikishirikishwa katika maswala mazima ya kibiashara katika ligi yetu, kusudi baadaye isijekuleta ukakasi na wasiwasi kama iliyotokea msimu huu "

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news