Orodha ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) 2022

NA DIRAMAKINI

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetoa wito kwa vijana waliohitimu elimu ya Sekondari Kidato cha Sita mwaka 2022 kutoka shule za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya jeshi hilo kwa mujibu wa sheria.

Vijana hao wamepangiwa kuripoti kambini kuanzia Juni 3 hadi 17, mwaka huu katika kambi mbalimbali ikiwemo Kambi ya JKT Rwamkoma mkoani Mara, JKT Msange Tabora,JKT Ruvu Pwani,JKT Mpwapwa na Makutupora JKT Dodoma.

Mkuu wa Tawi la Utalawa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena Mei 31,2022 jijini Dar es Salaam amesema, kambi nyingine vijana hao watakayo kwenda ni JKT Mafinga Iringa,JKT Mlale Ruvuma,JKT Mgambo,JKT Maramba mkoni Tanga,JKT Makuyuni Arusha, JKT Bulombora,JKT Kanembwa,JKT Mtabika mkoani Kigoma.

Ametaja kambi nyingine ni JKT Itaka Songwe,JKT Luwa,JKT Milundikwa Rukwa,JKT Nachingwea Lindi ,JKT Kibiti Pwani pamoja na Oljoro JKT Arusha.
”Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo,”amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema, jeshi hilo linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa mbalimbali huku orodha kamili ya majina ya vijana hao walioitwa makambi ya JKT yapo katika tovuti ya jeshi hilo.

Amesema, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo,umoja wa kitaifa,stadi za kazi,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa.

Post a Comment

0 Comments