Orodha ya walioitwa kwenye usaili nafasi za kazi Halmashauri ya Bagamoyo

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Shauri Selenda anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kupitia tangazo lenye kumb.Na.HWB/A.20/26/VOL.1/15 la tarehe 24/05/2022 kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Julai 4 hadi Julai 5,2022.

Usaili huo utafanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bagamoyo na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji huyo, wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo;

Mosi, usaili wa vitendo na mahojiano ya ana kwa ana utafanyika Julai 4, 2022 hadi Julai 5, 2022 katika Shule ya Sekondari Bagamoyo iliyopo Kata ya Dunda, Bagamoyo Mjini.

Pili kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi, tatu vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya Kusafiria.
 
Nne, wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha 1V,VI, leseni (kwa madereva) na Astashahada kutegemea na mahitaji ya tangazo la kazi na sifa ya mwombaji.

Tano, wasailiwa watakaowasilisha testimonials, provisional results, statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and form VI results slips) havitakubaliwa na hawataruhusiwa kuendelea na usaili.

Saba, kila msailiwa, atajigharamia kwa nauli, chakula, usafiri na malazi, Nane kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU,NACTE na NECTA).

Tisa, waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, Mkurugenzi Mtendaji amesema wanapaswa kutambua kuwa, hawakukidhi vigezo.
 
Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

Kumi, Mkurugenzi Mtendaji ameeleza kuwa, kila msailiwa anapaswa kuzingatia kufika na nakala ya kitambulisho cha NIDA; Wafuatao ndio wanapaswa kufika katika usaili huo;

Post a Comment

0 Comments