Rais Dkt.Mwinyi aelekea nchini Burundi, kumwakilisha Rais Samia miaka 60 ya Uhuru

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Burundi kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 60 ya nchi hiyo zinazotarajiwa kufanyika kesho Julai 1,2022.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dkt. Mwinyi aliagwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah. 

Rais Dkt. Mwinyi ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, katika safari yake hiyo amefuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo mkewe Mama Mariam Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi akifuatana na Mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na Maafisa mbalimbali wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akiagana na Mawaziri na viongozi mbalimbali wakati akiondoka kuelekea nchini Burundi kuhudhuria sherehe za miaka 60 ya nchi hiyo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Mama Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ikulu). 

Kesho Warundi wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 toka taifa hilo lilipojipatia uhuru wake toka kwa wakoloni wa Ubelgiji Julai 1, 1962.

Mwaka mmoja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa Umoja Mataifa, na chama mshindi kilikuwa UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore aliyemuoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili.

Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatia hali ya mvutano wa ukabila.

Mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urundi uhuru kamili, lakini kila nchi pekee kwa maana ya Jamhuri ya Burundi uhuru wake na Jamhuri ya Rwanda uhuru wake. Kwa sasa, mataifa hayo huru ni wa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaundwa na nchi wanachama saba.

Wengine ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kenya, Sudan Kusini, Uganda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku makao yake makuu yakiwa jijini Arusha, Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news