Serengeti Girls watua Dodoma 'Kiroyal Tour'

NA MWANDISHI WETU

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Fainali za Kombe la Doka la Dunia kwa Wanawake U17, Serengeti Girls, wametua Dodoma asubuhi hii, tayari kupokewa kifalme Bungeni Dodoma leo.
Kwa sadfa pia, leo ndio Siku ya Bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, bajeti inayosubiriwa kwa hamu katika kuonesha mwendelezo wa mageuzi makubwa anayoyafanya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta hizo.

Wakiwa katika suti zao kali, Serengeti Girls, watakaoiwakilisha nchi kwenye fainali hizo nchini India Novemba mwaka huu, baadaye leo watapokewa Bungeni Dodoma kwa kishindo.

Post a Comment

0 Comments