Serikali yakoleza kasi ya kufikisha maji vijijini, DC Abdala azindua mradi Mkoko

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Zainabu Abdala amezindua mradi wa maji kwenye Kijiji cha Mkoko uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 348.4 na utahudumia wakazi zaidi ya 1,600 wa kijiji hicho.
Abdala ambaye alizindua mradi huo wa maji chini ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwenye kijiji hicho cha Mkoko na Kitongoji cha Mtoni na kutembelea ujenzi wa mradi wa maji wa Fukayosi pia ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa kuikabidhi Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuendelea na hatua ya uendeshaji wa miradi hiyo.

Amesema, ameridhishwa na miradi hiyo na kupongeza mahusiano mazuri ya taasisi hizo kwani wanakwenda kuondokana na kero ya kunywa maji machafu yasiyo salama kiafya pamoja na kuliwa na mamba katika mto Wami.

Aidha, amesema kuwa RUWASA imepokea fedha za UVIKO-19 kutekeleza miradi nane kati ya hiyo ni mradi wa Mkoko ambao mkandarasi Lukedan Contractor amemaliza ujenzi kabla ya muda. 

Awali Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bagamoyo, James Kionaumela amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kupitia fedha za Uviko19 ilianza utekelezaji wa mradi huo. 

Kionaumela amesema kuwa, mradi wa Fukayosi umetekelezwa kwa fedha za UVIKO-19 kwa gharama zaidi ya milioni 350 ambapo ujenzi umefikia asilimia 95 , wanatarajia kaya 374 kupata huduma ya maji na Lengo ni kusaidia wananchi 2,242 ambao huduma haijawafikia ikiwemo vitongoji vya Umasaini na Lusako.

Wakazi wa Kijiji hicho wakiwemo Huruka na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkoko,Mtoro Masimba wamesema walikuwa wakipata shida ya maji kwa kuyapata mtoni ambapo walikuwa wakiliwa na mamba

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya LUKEDAN, Mhandisi Danny Amata ambao ndio wajenzi wa mradi huo ameishukuru Serikali kwa fursa hiyo kama mkandarasi wa ndani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news