USHIRIKA SIMIYU MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

NA DIRAMAKINI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) imemfikisha Katibu wa Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) cha Mbaragane katika Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu,Samwel Makeja katika mahakama ya wilaya hiyo kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi.

Katibu huyo amesomewa mashitaka yake yanayomkabili mahakamani hapo leo ambayo ni ubadhirifu wa fedha na kuchepusha fedha

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Albertina Mwigilwa ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,Chirstian Rugumila kuwa Mshtakiwa alitenda makosa hayo Oktoba 4, mwaka 2021 katika Wilaya ya Maswa.

Mwendesha Mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa, kosa la kwanza ni kwamba mshitakiwa akiwa Katibu wa AMCOS ya Mbaragane alifanya ubadhilifu shilingi 2,000,000 ambazo alipaswa kulipia ushuru wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU) katika musimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022.

Amesema, kosa hilo ni kinyume ya kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 marejeo ya mwaka 2019.

Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa katka kosa la pili mshtakiwa alichepusha fedha hizo kwa madhumuni yake binafsi kinyume na kifungu cha 29 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2019.

Mshitakiwa mara baada ya kusomewa mashitaka hayo aliyakana na hivyo kesi kupangwa tena Juni 24,mwaka huu ambapo atasomewa hoja za awali kwani upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news