'Tuache kutupa chupa za plastiki ovyo, ni uchafuzi wa mazingira'

NA SHEILA KATIKA

WANANCHI wametakiwa kuacha kutupa chupa za plastiki ovyo kwani kufanya hivyo ni uchafuzi wa mazingira.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Usimamizi wa Mazingira  na Maendeleo (EMEDO), Editrudith Lukanga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani. 

Hayo yamesemwa na Meneja mradi wa Shirika lisilo la kiserikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO), Arthur Mugema wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Mwanza.

Amesema,  kila mtu ana wajibu wa kulinda na kutunza mazingira ili yawe katika hali ya usafi.

Amesema, kupitia kampeni ya kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa taka za plastiki shirika hilo limetoa ajira kwa watu 24 ambao wanakusanya chupa za plastiki ili ziweze kutumika kwenye kazi mbalimbali za kijamii.

"Baada ya kuona chupa nyingi zimezagaa kwenye mitaa na kupelekea uchafu wa mazingira ndipo tulipoanza kuzikusanya kwani tumetoa ajira kwa watu 24 ambao wanatuletea chupa,"amesema.
Meneja mipango (program meneja)wa Shirika lisilo la kiserikali la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo(EMEDO)Arthur Mugema akiwaonyesha waandishi wa habari kituo cha taarifa na maarifa ya mazingira kilichojengwa kwa kutumia makopo ya plastiki 3600 kupitia kampeni ya kupunguza uchafu wa Mazingira Kwa taka za plastiki.

"Inasikitisha kuona watu hawatambui umuhimu wa chupa za plastiki, kwani zina umuhimu unaweza kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo kujenga banda la kupumzikia,kutengeneza mapambo mbalimbali na chupa hiyo unaweza kupanda mboga za majani na kujipatia kipato ni vema kuchangamkia fursa hii,"amesema Mugema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo,Editrudith Lukanga amesema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali ya usafi.

"Tunakusanya chupa za plastiki kwenye kaya mbalimbali lengo letu ni kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali ya usafi,"amesema Lukanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news