'Tupo tayari kuhesabiwa sisi kama Viongozi wa Dini pamoja na Waumini wetu'


NA DIRAMAKINI

MKUTANO wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022. 

Mkutano huu umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi. 
Katika mkutano huu; Viongozi wa Dini wameahidi kushiriki kwenye Sensa pamoja na kuwaelimisha na kuwahamasisha waumini wao kujitokeza kuhesabiwa.
"Tupo tayari kuhesabiwa sisi kama Viongozi wa Dini pamoja na Waumini wetu," wamesema kwa kauli moja Viongozi wa Dini ambao ndio wajumbe wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano.

Sensa ya Watu na Makazi itafanyika tarehe 23 Agosti, 2022. Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa.

Post a Comment

0 Comments