Waziri Bashungwa aahidi ushirikiano Miradi ya Maji katika Miji 28

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI itashirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Maji katika utekelezaji na usimamizi wa miradi wa maji ya miji 28 ili endelea kuleta mabadiliko nchini kwa kumtua mama ndoo kichwani.

“Nitumie nafasi hii kukuhakikishia Mhe.Rais OR-TAMISEMI kupitia Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri tutashirikiana na Wizara ya Maji katika kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa viwango;
Hayo yamebainishwa Juni 6, 2022 katika hafla ya uwekaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji ya Miji 28 kati ya Wizara ya Maji na Wakandarasi walioshinda zabuni iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Aidha, Bashungwa amempongeza Mhe.Rais kwa kuendelea kumtua mama ndoo kichwani akisisitiza kuwa azima ya Serikali ni kuhakikisha inaboresha maisha ya Mtanzania, lakini pia kuwaondolea adha wanafunzi hasa wa kike kutumia muda mrefu kuchota maji badala ya kusoma na kufanya mapitio ya masomo yao,hivyo OR-TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Maji katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha hiyo.

“Tunakushukuru na kukupongeza kwa kuweka jitihada kubwa ya kuhakikisha dhamira yako ya kuwatua ndoo wakina mama pamoja na watoto ambao wakitoka shule wanashindwa kusoma na kufanya mapitio ya masomo yao na kwenda kuchota maji inatekelezwa , tunaona kila siku kunapokuchwa unaendelea kumtua mama ndoo kichwani,”amesema Waziri Bashungwa.

Kwa upande mwingine Bashungwa amempongeza Waziri wa Maji, Mhe. Juma Awesso kwa kuwa mbunifu katika utekelezaji wa miradi ya maji ya Miji 28 amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI ipo tayari kutoa ushirikiano katika kutekeleza miradi hiyo yenye lengo la kuleta mabadiliko nchini.

“Nikupongeze Waziri wa Maji, Wizara ya Maji hakunaga jambo dogo kila siku ni jambo kubwa OR-TAMISEMI inakupongeza kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais katika kutekeleza adha ya kumtua mama ndoo kichwani lakini pia ni wabunifu tunaona jinsi mnavyounganisha kazi pamoja na Sanaa katika kufikisha ujumbe na sisi tuna mengi ya kujifunza kutoka kwenu,”amesema Bashungwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news