Waziri Mkuu atoa siku tano kwa Wizara ya Kilimo, asema haikubaliki

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tano kuanzia leo Juni 8, 2022 hadi Juni 12, 2022 Wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote wizarani hapo na kuzikabidhi kwa wakurugenzi.

“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko. Jumapili saa 10 jioni ziwe zimefika kwa wahusuka.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Profesa Siza Tumbo (kushoto) wakati alipokagua pikipiki zilizopo katika Ofisi za Wizara ya hiyo Juni 8, 2022 jijini Dodoma, ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Maafisa Ugani kote nchini. Waziri Mkuu ameiagiza Wizara hiyo kuhakikisha ifikapo Juni 12, 2022 (jumapili) ziwe zimeshakabidhiwa kwa Maafisa Ugani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ametoa agizo hilo leo Juni 8, 2022 alipokagua Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo eneo la VETA, Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ugani zikiendelea kuwepo.

Aprili 4, 2022 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ugawaji wa vitendea kazi vilivyoandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Maafisa Ugani wote nchini. Vifaa ni pamoja na pikipiki.

Amesema tayari Mheshimiwa Rais Samia alishazikabidhi kwa ajili ya kupelekwa kwa maafisa ugani, hivyo kitendo cha pikipiki hizo kuendelea kubaki katika eneo hilo hakikubaliki.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamepokea maelezo hayo na watayafanyia kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news