Wizara ya Maji, wadau kukutana Dar kesho

NA GODFREY NNKO

WIZARA ya Maji kwa kushirikiana na Taasisi ya 2030 ya Water Resources Group, Global Water Partnership Tanzania na Ubalozi wa Canada nchini Tanzania wameandaa Mkutano wa Tano wa Jukwaa la Taifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji (National Multi-Sectoral Water Resources Management and Development Forum).
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ambapo amefafanua kuwa, mkutano huo utafanyika Juni 18, 2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Sanga amesema, kauli mbiu ya mkutano huo ni "Thamani ya Maji-Mchango wa Rasilimali za Maji Kwenye Uchumi wa Taifa"- (The Value of Water-Contribution of Water Resources in the Country's Economy).


Post a Comment

0 Comments