Bei ya Dizeli, Petroli, mafuta ya taa juu

NA DIRAMAKINI

BEI ya mafuta imepanda tena mwezi huu na kuivuka ile ya Mei, iliyokuwa kubwa zaidi katika historia ya Tanzania kiasi cha kuilazimu Serikali kutoa ruzuku.

Mei, bei ya petroli ilifika shilingi 3,148 jijini Dar es Salaam ikipanda kwa shilingi 287 kutoka Aprili kwa kila lita moja huku dizeli ikipanda kwa shilingi 566 kutoka shilingi 2,692 hadi shilingi 3,258 katika kipindi hicho.

Katika taarifa iliyotolewa Julai 5, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), bei ya rejareja jijini Dar es Salaam itakuwa shilingi 3,220 kwa lita moja ya Petroli na shilingi 3,143 kwa Dizeli huku mafuta ya taa yakifika shilingi 3,442.

EWURA imesema, bei hizi mpya ambazo zimejumuisha ruzuku ya shilingi bilioni 100 iliyotolewa na Serikali zinaanza leo, kama kusingekuwepo ruzuku hiyo lita ya petroli ingeuzwa shilingi 3,497 na dizeli shilingi 3,510 jijini Dar es Salaam wakati Kyerwa ingekuwa shilingi 3,735 kwa petroli na shilingi 3,748 kwa dizeli ambapo mafuta ya taa hayana ruzuku.
"Katika kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta hapa nchini Serikali imetoa ruzuku nyingi ya shilingi bilioni 100 kwa mwezi Julai. Ruzuku hiyo imeelekezwa katika mafuta ya petroli na dizeli na kiasi kikubwa kimeelekezwa katika dizeli kwa lengo la kudhibiti mfumko wa bei," imeeleza taarifa ya EWURA.

Mwezi uliopita, lita ya petrol iliuzwa shilingi 2,994 na dizeli shilingi 3,131 mkoani Dar es Salaam huku Kyerwa ikiwa shilingi 3,539 kwa petroli na shilingi 3,232 kwa lita ya dizeli.
 
Mwezi Juni

 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news