Bosi Vunjabei achukua fomu Wazazi CCM Iringa

NA DIRAMAKINI

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Bw.Fadhil Fabian Ngajilo leo amejitosa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Uwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi mkoani hapa.
Ngajilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vunjabei Ltd amechukua fomu hiyo leo Julai 2, 2022 mkoani Iringa.

Kada huyo aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa kati ya mwaka 2008 hadi 2012.
Baada ya kuiongoza jumuiya hiyo kwa mafanikio, pia mwaka 2020 alijitosa kuwania ubunge na kushika namba tatu kati ya wagombea 52.

Bw.Ngajilo mbali na kujihusisha katika siasa mkoani Iringa pia ni miongoni mwa wadau muhimu wa maendeleo ambao mara kwa mara amekuwa akishiriki shughuli za maendeleo ikiwemo kijamii, kiuchumi na michezo.

Post a Comment

0 Comments