Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Julai 25,2022


Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Simon Sirro amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua katika wadhifa huo na kuahidi kwenda kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.

Aidha, Balozi Sirro amewaomba Watanzania kumuombea Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi (IGP), Camilius Wambura pamoja na timu yake ili waweze kutimiza majukumu yao vema kwa manufaa ya nchi.

Sirro ameyasema hayo Julai 24, 2022 kwenye misa ya shukrani aliyoifanya kijijini kwao katika Kanisa Katoliki Muriaza, Jimbo la Musoma Mkoa wa Mara.

Amefanya misa hiyo ikiwa ni siku takribani tano zimepita tangu Rais Samia kufanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi, Julai 19 2022 na kumbadilishia majukumu.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia alimteua Camilius Wambura aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa IGP kuchukua nafasi ya Sirro ambaye aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe.

IGP Wambura na Balozi Sirro kwa pamoja waliapishwa Julai 20, 2022 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments