JWTZ washiriki mashindano ya majeshi duniani

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) inashiriki mashindano ya Dunia kwa Timu za Majeshi (CISM) yanayoendelea mjini Warendorf nchini Ujerumani. 

Mashindano hayo ya majeshi yanafanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu timu 16 zimeshiriki mashindano haya yanayoendelea nchini Ujerumbani ambapo Timu ya Jeshi kutoka Tanzania imewakilishwa na Timu ya Mpira wa Kikapu Wanaume na Timu ya mpira wa Kikapu Wanawake. Mashindano haya yameanza rasmi Julai 5, 2022 ikishirikisha timu za majeshi toka Bangladesh, Canada, Cyprus, Ufaransa,Ujerumani, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Mongolia, Morocco, Netherlands, Jamhuri ya Korea, Saudia Arabia, Slovenia, Marekani na Tanzania. 

Mashindano haya yanaendelea katika hatua ya mchujo ambapo Timu ya Jeshi toka Tanzania imepangwa kundi D ikijumuishwa na Uholanzi, Ujerumani, Luxembourg na Bangladesh kwa timu ya mchezo wa kikapu wanaume. 

Kwa upande wa Timu ya Jeshi Wanawake imepangwa katika kundi pamoja na Marekani, Ujerumani, Canada, Uholanzi na Latvia.

Timu hizo za jeshi zimeundwa na Wachezaji kutoka NGOME na JKT na Meneja wa Timu ni Kapteni Mohamed Kasui, mashindano hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 10, 2022 mjini warendorf nchini Ujerumani.

Post a Comment

0 Comments