Mambo nane aliyoyasisitiza Mwenyekiti wa TEF, Balile kuhusu mchakato maboresho ya sheria

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile amesisitiza kuwa,wadau wa Sekta ya Habari nchini wana imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Amesema, Mheshimiwa Rais kupitia serikali anayoiongoza ameonesha nuru njema katika tasnia hiyo, hivyo hata katika mchakato unaoendelea wa kuzifanyia mapitio sheria mbalimbali zinazohusiana na habari nchini utakwenda kwa kasi ili maboresho yafanyike mapema. Zifuatazo ni nukuu muhimu nane zinazotoka kwa Bw.Balile;

1>"Kwanza tunaishukuru Serikali baada ya kuwa tumewasilisha ile compound (mjumuisho) ya maoni ya wadau, Serikali iliyapokea na ikaanza kuyafanyia kazi, lakini pia Mheshimiwa Rais amekuwa akitoa msukumo mkubwa sana akisema kwamba tuhakikishe hizi sheria zinashirikisha wadau washirikiane na Serikali kuhakikisha kwamba zinaboreshwa.

2>"Tulikwenda vizuri hapo mwanzo, lakini tangu baada ya Mei tunaona kasi imepungua kidogo tungependa kujua wizara ilikuwa imepanga kunakuwepo na mikutano kadhaa na tujadiliane na wataalamu. Lakini kwa sasa tunaona kama kila kitu kimesimama, na tunaendelea kuuliza tunaambiwa mikutano bado ipo. Nadhani bado tunahizitaji sheria na tunahitaji haya mabadiliko ya haraka kadri inavyowezekana kuliko wakati wowote. 

3>"Tukipitwa lile bunge la mwezi wa tisa inamaana tutasubiria mwaka mmoja mwingine mmoja kwa sababu bunge la mwezi wa tisa kwa kawaida ndilo bunge la miswaada. Inawezekana tukaenda mwezi wa tisa au wa 11, lakini kama utashi uko kwenye wizara yenye dhamana, tunachotafuta zaidi ni haki ya kupata habari na uhuru wa vyombo vya habari.

4>"Na huu uhuru unawezesha haki nyingine kupatikana, kwa hiyo demokrasia na vitu vingine vinavyozungumzwa vinatokana na uhuru wa watu kutoa mawazo na kutoa taarifa. Inapokuwa uhuru haujalindwa kisheria, unachelewesha hivi vingine kupatikana katika jamii.

5>"Vifungu ni vingi, Mahakama ya Afrika Mashariki iliamua vifungu 16, lakini tunadhani tupitie kwa pamoja kuanzia kifungu cha 1-67 na zipo sheria nyingine nyingi ukiangalia ile Sheria ya EPOCA na nyingine nazo zinahitaji marekebisho ya hapa na pale ili kwa pamoja tuwe na sheria ambazo hazikinzani na utaratibu wa msingi wa haki ya kupata taarifa kama inavyokubalika duniani ni mjadala na ni mchakato ambao tunapaswa kushirikishana tulio wengi kwa pamoja.

5>"Tunaangalia utashi wa kisiasa kwamba, wakati ule uongozi uliokuwepo na uongozi uliopo sasa wa Rais Samia Hassan ni tofauti na hii inatupa matumaini makubwa.

6>"Tunaomba Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya habari ahakikishe mchakato huu haukwami. Kama alivyokuwa akizungumza mara kwa mara sasa zile kauli zake tuzione kwenye vitendo, ukizungumza naye Mheshimiwa Waziri anakwambia kila kitu kitakwenda sawa. Wataalamu wanakwambia kila kitu kinakwenda ila tunaona muda unapita hakuna kinachotokea," amesema Balile.

7>"Sasa matumanini tunaweza kuendelea kuyashikilia, lakini mwisho tukajikuta tunafika mwisho tukiwa na kasha lisilo na matunda.

8>"Kwa sasa sisi wadau tunaendelea na uzengezi (advocacy) tunafanya ushawishi tunaendelea kuwasiliana na Serikali na tunaamini kwamba tutafikia hiyo hatua bado tunayo matumaini, hatujakata tamaa,"amesema Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news