Mheshimiwa Simbachawene atoa maagizo Mpwapwa

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuisajili kwa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) barabara ya Kikuyu Mangaliza kuelekea Kijiji cha Kilambo. 
“Tujenge misingi imara katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili tuimarishe ujenzi wa miundombinu ya barabara, miundobinu ya afya na miundo mbinu ya elimu,”amesema. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Maturi jimbo la kibwake Halmashauiri ya Mpwapwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kata ya Mangaliza katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua miundo mbinu ya ujenz wa madarasa katika shule ya msingi Mangaliza jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

Post a Comment

0 Comments