Mheshimiwa Simbachawene awapongeza wananchi Kibakwe kwa kujikita katika shughuli za maendeleo

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene amesema, katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 10 kwa Halmashauri ya Mpwapwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Unapopeleka fedha kwa wananchi kule chini, kule chini ndio kuna changamoto na wananchi wetu ndio wanapata maendeleo, miradi hii tuliyopewa mwaka jana lazima tuitekeleze kwa kasi kubwa, ili zinapokuja fedha nyingine tuendelee kutekeleza miradi;
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibakwe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tarafa ya Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb), Mhe. George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe wakati akihutubia wananchi wa Jimbo la Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

“Wananchi wa Mpwapwa sasa wanazungumza kuhusu maendeleo nawapongeza kwa kuwa wanaharakati wa maendeleo,"amesema Mhe.Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Josephat Maganga alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Mhe.George Simbachawene akizungumza na halaiki ya wananchi walijitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpwapwa, Bi, Mwanahamisi Ally katika mkutano wa hadhara ulioufanyika Tarafa ya Kibakwe katika Halmashauri ya Mpwapwa.

Aidha, Mhe. Simbachawene amewahakikisha wananchi wa Kata Kibakwe kwamba jokofu kwa ajili ya kuhifadhi maiti lipo, katika gharama za ujenzi wa kituo cha afya Kibakwe. 

Naye Diwani wa Kata ya Kibakwe, Mhe. David Atanas amepongeza jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe katika kuletea wananchi maendeleo, amesema Kibakwe imepata shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi miundombinu ya maji katika jimbo la Kibakwe na ujenzi wa barabara kwa umbali wa kilomita moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news