Mke wa Rais wa Zanzibar,Mariam Mwinyi awapa tabasamu wazee

Mshauri wa Rais wa masuala ya Siasa, Mhe.Ali Salum Haji (Kirova) alipokuwa akitoa salamu kwa niaba ya Mke wa Rais Mama Mariam Mwinyi wakati wa kutoa mkono wa Idd El Hajj kwa wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Mjini Magharibi ikiwa ni utaratibu wake Mke wa Rais kila ifikapo Kipindi cha Sikukuu kwa Wazee hao leo Julai 10,2022.(Picha na Ikulu). Afisa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Rais Ikulu, Khadija Pembe Juma akitoa Mkono wa Idd el Hajj kama Sikuu ya Wazee wanaoishi nyumba za Wazee Sebleni kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi,ambapo ni utaratibu wake kila ifikapo kipindi k ichi kipindi cha Sikukuu kwa Wazee hao. Wazee kinamama wanaoishi katika Nyumba za Wazee Sebleni wakipokea mkono wa Idd el Hajj ikiwa ni utaratibu wa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi, kwa niaba yake Afisa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Rais Ikulu Khadija Pembe Juma, akitoa mkono wa Idd el Hajj kwa wazee hao leo.[Picha na Ikulu] 10 julai 2022. Wazee kinamama na Kinababa wanaoishi katika Nyumba za Wazee Sebleni wakiitikia dua iliyoombwa mara kupokea mkono wa Idd El HaJJ ikiwa ni sikukuu yao iliyotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi, hafla iliyofanyika leo katika makazi yao Sebleni Wilaya ya Mjini. Wazee wanaoishi Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini wakisikiliza kwa makini salamu za Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi (hayupo pichani) zilizotolewa kwa niaba yake na mshauri wa Rais Siasa Mhe.Ali Salum Haji (Kirova) wakati wa Utoaji wa mkono wa Idd kwa wazee hao leo. Mzee Maria Kurwa Maziku, anayeishi katika Nyumba za Wazee Welezo akipokea Mkono wa Idd el Hajj ikiashiria Sikuu ya Wazee wanaoishi nyumba za Welezo, kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi,Afisa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Rais Ikulu Khadija Pembe Juma, akitoa mkono wa Idd mbapo ni kawaida yake Mke wa Rais,kila ifikapo kipindi cha Sikukuu kutoa Mkono wa Idd kwa Wazee hao.Wazee wanaoishi katika Nyumba za Wazee Welezo ni miongozni mwa wazee waliopokea mkono wa Idd El Hajj ikiwa ni sikukuu yao iliyotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi, hafla iliyofanyika leo katika makazi yao Welezo Wilaya ya Mjini.

Post a Comment

0 Comments