Prof.Kahyarara:Biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Godius Kahyarara amesema biashara kati ya Tanzania na Kenya imekuwa zaidi baada ya ya makubaliano kati ya Tanzania na Kenya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru 49 kati ya 64 wakati vikwazo vingine 15 vilivyobaki vinafanyiwa kazi. 
Prof. Kahyarara ameyasema hayo leo Julai 6, 2022 wakati wa kipindi cha Morning Trumpet kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha Azam jijini Dar es Salaam.

Amesema, katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, uwekezaji umeongezeka kutoka bilioni 1 hadi bilioni 9 na Kituo cha Uwekezaji kimesajili wawekezaji 380 wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza mpango wa kuboresha mazingira ya biashara kwa kufuta tozo na kufanya marekebisho ya sera na sheria mbalimbali ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiasha nchini na kuongeza ajira, pato la taifa na kukuza uchumi kwa ujumla. 

Akitolea mfano wa kongani ya viwanda ya Kwala iliyopo Kibaha inayotarajiwa kutoa ajira 100,000 za moja kwa moja na 500,000 zisizo za moja kwa moja, Prof. Kahyarara amesema, Serikali inalenga kuwa na viwanda vikubwa vingi vitakavyoanzishwa katika kongani za viwanda mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza ajira, pato la taifa na mauzo ya nje. 

Aidha, amesema Serikali imeanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Huduma za pamoja kwa Wawekezaji unaounganisha taasisi 12 zinazohusika kuhudumia wawekezaji ili kupunguza urasimu na changamoto mbalimbali katika uwekezaji na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Pamoja na Mfumo huo, Serikali pia imeanzisha Mfumo unaroa huduma za uhamiaji kwa mtandao hususan utoaji wa vibali vya Ukaazi (e-Permit) na Vibali vya kufanya kazi nchini kwa kuzingatia soko la ajira.

Katika kutatua changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula, Prof.Kahyarara pia amesema Serikali inachukua hatua mbalimbali za kuongeza uzalishaji wa mazao yanayotoa mafuta ya kula pamoja na kuwawezesha wananchi kumiliki viwanda vidogo na vya kati vya kuchakata mafuta hayo kupitia Programu maalumu ya Total Industrial Solution inayowawezesha wananchi kumili kiwanda ndani ya muda mfupi kwa gharama nafuu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news