REA yaeleza ilivyoboresha maisha ya wananchi vijijini

NA VERONICA SIMBA-REA

MIRADI ya umeme vijijini inayoendelea kutekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imechangia kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo hayo.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu na Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela, wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa leo Julai 3, 2022 jijini Dar es Salaam. (Picha zote na VERONICA SIMBA-REA).

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari. 

Akizungumza katika Banda la REA lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba), Mhandisi Olotu amesema, umeme vijijini umewapatia wananchi fursa ya kufanya kazi mbalimbali za ujasiriamali hivyo kujiongezea kipato.Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Francis Songela (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (kulia), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mjasiriamali anayeuza majiko yanayotumia nishati kidogo, wakati wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, Julai 3, 2022 jijini Dar es Salaam.

Amezitaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni pamoja na kuchomelea vyuma, saluni za kike na kiume pamoja na mashine za kusaga nafaka.

Aidha, ameongeza kuwa upatikanaji wa umeme vijijini umewezesha kuboresha huduma mbalimbali zitolewazo kwa umma ikiwemo afya na elimu. 
Mtaalamu kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Michael Kyessi (kulia), Akifafanua jambo kwa Mdau wakati wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, Julai 3, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akisaini Kitabu cha Wageni, alipotembelea Banda la REA katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, Julai 3, 2022 jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Francis Songela, amesema kwamba REA imejipanga kuhakikisha inafikisha nishati hiyo katika maeneo yote vijijini, awamu kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. 

Akifafanua, Mhandisi Songela amesema REA inatambua kiu kubwa ya umeme waliyonayo wananchi vijijini, ndiyo maana kazi ya kupeleka nishati hiyo ni endelevu ikilenga kuvifikia vijiji na vitongoji vyote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news