Serikali kufanya utafiti wa uanzishaji wa vitalu kwenye ukanda wa bahari

NA DIRAMAKINI

ILI kuongeza tija kwa viwanda vya uchakataji wa samaki Serikali inafanya utafiti wa uanzishaji wa vitalu kwenye ukanda wa bahari.

Hayo yamesemwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki wakati makabidhiano ya majengo ya ofisi za vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMU) kwenye soko la samaki Bagamoyo.
Ndaki amesema kuwa, kwa sasa viwanda vinazalisha kwa uwezo mdogo wa asilimia 30 hadi 40 ambapo inataka uzalishaji uongezeke kwa kuweka vitalu kwenye bahari.

Aidha, amesema upembuzi kwenye maziwa umefanyika kwenye mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita ambapo vitalu hivyo vitazinduliwa na watakabidhiwa wana vikundi kuendesha.

Naye Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa, wadau hao wanapaswa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na uvuvi haramu kwani hiyo ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Steven Lukanga amesema kuwa ,malengo ya ujenzi wa Masoko ya samaki kwenye Wilaya tano za Mkinga, Bagamoyo, Lindi Vijijini na Tanga Mjini ni kuboresha uvuvi wa samaki ambapo kuna vikundi 50.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Abdala amesema kuwa, wilaya hiyo inategemea mapato kutokana na uvuvi ambapo asilimia 30 ya mapato yanatokana na uvuvi na wameipa kipaumbele sekta ya Uvuvi ili kuboresha upatikanaji wa mapato na watakabiliana na uvuvi haramu ili kutoathiri mazao ya samaki. Jengo hilo la soko la samaki limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news