Serikali kujenga nyumba ya walimu Shule ya Sekondari Lumuma

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imeahidi kujenga nyumba ya walimu moja (two in one) itakayojengwa kwa kupitia mradi wa EP4R katika Shule ya Sekondari Lumuma iliyojengwa madarasa sita kwa nguvu za wananchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua ujenzi wa shimo la choo katika Sekondari ya Lumuma jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wananchi wa kata Lumuma baada ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo.

“Gharama za matofali katika ujenzi wa nyumba hiyo ya walimu zitatolewa na nguvu kazi ya wananchi, na tunaweza kujenga nyumba mbili za aina hiyo kama tutakaza msuli vizuri," alisema Waziri.
Kupitia fedha za mfuko wa jimbo nitasaidia katika kukamilisha ujenzi wa miundo mbinu mingine, ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya madarasa katika shule ya sekondari Lumuma jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa. 

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri ameelekeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kusajili barabara ambazo hazijasajiliwa hasa zinazoenda kwenye maeneo ya huduma za kijamii au maeneo mapya ya utawala ambayo yameongezeka.

Halmashauri inapaswa kuzifungua na kisha kuzisajili kwa mujibu wa mchakato wa kisheria, ambapo lazima kamati ya maendeleo ya kata ikae na kuzibainisha baraba mahali zilipo na urefu wake na kuonesha taasisi inayokwenda ili kupeleka mapendekezo kwenye Halmashauri na baadae kupeleka DCC na baadae kwenye bodi ya barabara ya mkoa ( Road Board).

“Barabara hizi zikisajiliwa kwa mujibu wa sheria ni rahisi kwa wakala wa barabara vijijini (TARURA) kuzitambua na kuzitengea fedha,"alisema Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua ujenzi wa shimo la choo katika sekondari ya Lumuma jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa. 

Awali katika taarifa yake Diwani wa Kata ya Lumuma, Mhe. Joktan Chelligah amesema wananchi wa kata ya Lumuma wamejenga shule hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Wananchi tumechanga fedha kiasi cha milioni 17, lakini Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imetuchangia milioni 20, na mifuko 150 ya saruji pamoja na mabati 250, na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma kimechangia mifuko 130,”alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news